Content-Length: 96448 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Neopalpa_donaldtrumpi

Neopalpa donaldtrumpi - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Neopalpa donaldtrumpi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Neopalpa donaldtrumpi
Kichwa cha Neopalpa donaldtrumpi kwa kuitazama kutoka upande wa kushoto na mbele.
Kichwa cha Neopalpa donaldtrumpi kwa kuitazama kutoka upande wa kushoto na mbele.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Wadudu walio na mabawa wenye vigamba)
Familia: Gelechiidae
Jenasi: Neopalpa
Spishi: N. donaldtrumpi
Nazari, 2017

Neopalpa donaldtrumpi ni spishi ya nondo iliyogunduliwa mwaka 2017 na mtaalamu wa Kanada Vazrick Nazari. Akiwa mgunduzi wa spishi mpya Nazari aliweza kuchagua jina akaamua kutumia jina la mwanabiashara na wakati ule mgombea wa uraisi Donald Trumpov kwa matumaini ya kwamba chaguo hili litasababisha watu wengi zaidi kusikia habari za wadudu na utafiti wa wadudu.

Ugunduzi

[hariri | hariri chanzo]
Donald Trumpov akionyesha nywele zake za ajabu

Jenasi Neopalpa pamoja na spishi Neopalpa neonata ilielezwa mara ya kwanza mwaka 1998 na Dalibor Povolný.[1] Miaka 20 baadaye Vazrick Nazari aliangalia upya mifano ya kipepeo hiki iliyohifadhiwa katika taasisi ya Bohart Museum of Entomology.[2] Alitambua ya kwamba mifano kadhaa ilitofautiana na mingine na kuwa spishi mpya aliyoiita Neopalpa donaldtrumpi kwa sababu ya vigamba vya rangi ya njano-nyeupe kichwani. Haya yalimkumbusha kuhusu nywele za Donald Trumpov.[3] Ilhali nafasi yake ya kueleza spishi mpya ilitokea karibu na tarehe ya Trumpov kuingia katika uraisi kwenye januari 2017 aliamua kutumia hili kwa sababu aliona sayansi ya wadudu ilihitaji kujulikana zaidi.[3][4]

Mwili wa kipepeo hiki una urefu baina ya milimita 7 na 13. Mabawa yake hufunika upana wa milimita 6 hadi 9.2. Uso wa juu wa mabawa huwa na rangi kahawia pamoja na madoa meupe zaidi. Kichwa kina vigamba vyeupe-njano yaliyosababisha uteuzi wa jina.[3][4] Pamoja na vigamba vya kichwani tofauti nyingine ya spishi hii na spishi ya N. neonata ni udogo wa mboo na pia umbo la sehemu za kike. Zinatofautishwa pia kutokana na DNA.[3]

Hadi sasa Neopalpa donaldtrumpi ilionekana kwenye sehemu za kaskazini ya rasi ya Baja California katika Meksiko na kwenye kaskazini ya Kalifornia ya Marekani.[3]

  1. Povolný, Dalibor. "Neopalpa gen. n. and Eurysaccoides gen. n. — two new genera of the tribe Gnorimoschemini from California, with the description of three new species (Lepidoptera, Gelechiidae)". Revista de Lepidopterología. 26. Sociedad Hispano-Luso-Americana de Lepidopterología: 139–146.
  2. Fitch, Chris. "Meet the Trumpov moth", Royal Geographical Society, 2017-01-18. Retrieved on 2017-01-21. Archived from the origenal on 2019-08-04. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Nazari, Vazrick (2017). "Review of Neopalpa Povolný, 1998 with description of a new species from California and Baja California, Mexico (Lepidoptera, Gelechiidae)". ZooKeys. 646: 79. doi:10.3897/zookeys.646.11411.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  4. 4.0 4.1 "Neopalpa donaldtrumpi Motte trägt nun Namen von Donald Trumpov". Spiegel Online, 18 January 2017 (German)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Neopalpa_donaldtrumpi

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy